Taasisi ya Kiislamu inayojikita katika kutoa elimu bora, kusaidia jamii, na kuendeleza maadili ya Kiislamu nchini Tanzania.
Al-Khairiya Islamic Foundation imeanzishwa mnamo tarehe 28/01/2022 Tanzania ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, wilaya ya Kigamboni. Ilianza ikiwa na wanachama 16, na hadi tarehe 19/03/2023 ilifikia wanachama 31. Taasisi ilipata usajili rasmi tarehe 21/03/2025 kwa namba ya usajili S.A 23853.
Kuwa taasisi bora ya Kiislamu nchini Tanzania inayochochea maendeleo ya elimu, afya, na ustawi wa jamii kwa misingi ya Uislamu na umoja wa kijamii.
Kutoa elimu bora ya Kiislamu, kusaidia makundi maalum kama yatima, wajane, na wazee, na kuendeleza miradi ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya jamii nzima.
Baada ya miaka mitatu (3), tunatarajia kufikia malengo yafuatayo:
Kujenga shule za Kiislamu kuanzia awali hadi chuo kikuu
Kuanzisha vituo vya afya na maabara
Kuanzisha vituo vya watoto yatima
Miradi ya kilimo na ufugaji
Kujenga madrasa na misikiti
Kusimamia elimu ya dini na jamii
Kusimamia mashindano ya Tahfidhi Qur'an kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa (2022-2024), na lengo la kufanya mashindano ya taifa mwaka 2025
Kutoa msaada kwa yatima, wajane, wazee, na watu wenye mahitaji maalum
Kuandaa semina, warsha, na makongamano ya kijamii na kidini
Kuanzisha na kuendeleza vyombo vya habari vya kidigitali kwa ajili ya elimu ya jamii
Tupo tayari kukusaidia. Wasiliana nasi kwa njia yoyote inayokufaa.
Wilaya ya Kigamboni, mtaa wa Ferry
Fremu za CCM, namba 28 na 29
Dar es Salaam, Tanzania
Bofya ramani hapo juu kupata maelekezo ya kufika ofisini mwetu